Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi kuchukuliwa na upepo na kupelekwa usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa ujumla.
Mithali 29: 18
Maono yako kwa ajili ya kazi ya Mungu ni lazima
yaendane na agizo kuu alilolitoa Bwana Yesu kwa wote wanaomwamini.
Marko 16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa
kila kiumbe.
Ni lazima mara zote agizo hili liwe ndani yako ili
unapoendelea na maono yako usijeenda mbali na agizo hili.
Shetani hujaribu kuyafisha maono yako na usipokuwa
mwangalifu atayapoteza kabisa. Yeye mara zote hutaka kituzuia kuyafanya mapenzi
ya Mungu, anajua akiyaua maono yetu hatutaweza kuifanya kazi ya Mungu kwa
ukamilifu.
2Korintho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda;
kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
Mambo yafuatayo shetani huyatumia kuua maono yetu:
2. Uhusiano uliovinjika katika mwili
wa Kristo
Tunaporuhusu makosa ya ndugu zetu katika Kristo kuzaa uchungu badala ya
kusamehe, tunaruhusu shetani kuyafunga macho yetu ya kiroho na hivyo kushindwa
kuiona njia ya kuelekea kwenye maono yetu.
3. Tamaa ya mambo
yanayoonekana
Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame
yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.
Ukiangalia sana mambo ya dunia na tamaa zake utajikuta
unayasahau maono yako na kubaki umefungwa na mambo hayo.
4. Kuangalia sana
mambo ya nyuma.
Unapoacha
kutazama mbele unapoelekea na kuweka nguvu na akili yako yote katika mambo ya
nyuma yaliyopita, utapoteza kusudi lako na maono yako.
Mwanzo 19:26 Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma
yake, akawa nguzo ya chumvi.
Wafilipi 3:13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba
nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma,
nikiyachuchumilia yaliyo mbele.
5. Kutumia muda
mwingi kuangalia matatizo
Shetani hujaribu kutufanya tuangalie tu matatizo
tuliyonayo na yale yanayoweza kutokea tunapoyafanyia kazi maono yetu hivyo
kutuondolea imani ya kuyakamilisha. Biblia katika kitabu cha hesabu inaelezea
habari za wapelelezi kumi waliorudi na habari za kukatisha tamaa katika
kuiendea nchi ya ahadi maana waliangalia zaidi matatizo na kupoteza maono yao
ya kuingia nchi ya ahadi.
Joshua na Kaleb waliona zaidi ya matatizo, waliuona
ukuu na uaminifu wa Mungu. Hawakuwa na hofu yoyote hivyo waliweza kuingia nchi
ya ahadi (kukamilisha maono yao) maana walimwamini Mungu. Petro alijaribu
kutembea juu ya maji lakini alipoona mawimbi akasahau Yesu aliyekuwa mbele yake
akimwambia njoo, akaweka akili kwenye mawimbi akaanza kuzama.
Ili tuweze kuyafanikisha maono yetu ni lazima tuwe na
uhusiano na ushirika wa karibu na Roho Mtakatifu.
Ubarikiwe na BWANA Yesu.
Post A Comment:
0 comments so far,add yours