Shalom

Je Mungu ni sehemu ya mazungumzo yako ya kila siku na watoto wako? Au unakwepa kuongea nao habari za Mungu? Watoto wako wanamuona Mungu katika maneno yako ya kila siku? Kitu unachokithanimi utawekeza muda wako, mali na hata nguvu zako. Watoto wako waone jinsi unavyowekeza kwa Mungu katika kulisoma neno lake, kuomba, kuhudhuria kanisani na kutumika katika kazi ya Mungu.

Tunapozungumza ukuu wa Mungu na watoto wetu katika maisha ya kila siku tunawajengea hazina kubwa ya imani kwa Mungu wao ambayo watakuwa nayo siku zote. Pamoja na kuwahamasisha kupata maksi nzuri darasani, kujihusisha na michezo na kufanya kazi za nyumbani hakikisha unawafundisha kumtumikia Mungu katika umri wowote walionao. Neno la Mungu liwe sehemu ya maisha yako na watoto wako siku zote.

KumbuKumbu 11:18-19 “Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohonu mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo yafunzeni Vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo“

 



Chanzo: https://womenofchrist.wordpress.com

Share To:
Magpress

Calvin Petro

Kwa Moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na Maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako Nisije nikakutenda dhambi. (Zaburi 119:10-11).

Post A Comment:

0 comments so far,add yours